1 Wathesalonike Chapter 5

For English

Read 1 Wathesalonike Chapter 5 Online

Read 1 Wathesalonike Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wathesalonike in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wathesalonike and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Wathesalonike 5

Sura 5

1. Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6. Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

7. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.

9. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;

10. ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.

11. Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.

12. Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;

13. mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.

14. Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.

15. Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

16. Furahini siku zote;

17. ombeni bila kukoma;

18. shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

19. Msimzimishe Roho;

20. msitweze unabii;

21. jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;

22. jitengeni na ubaya wa kila namna.

23. Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

24. Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.

25. Ndugu, tuombeeni.

26. Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.

27. Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu.

28. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

About 1 Wathesalonike Chapter 5

Read 1 Wathesalonike Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wathesalonike in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Wathesalonike
Chapter: 5
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wathesalonike. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Wathesalonike Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Wathesalonike Chapter 5?

1 Wathesalonike Chapter 5 is part of the Book of 1 Wathesalonike in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Wathesalonike Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-wathesalonike

  1. 1 Wathesalonike Chapter 2
  2. 1 Wathesalonike Chapter 4
  3. 1 Wathesalonike Chapter 3
  4. 1 Wathesalonike Chapter 1

Explore More from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 3
  2. Yohana Chapter 11
  3. Ufunuo wa Yohana Chapter 3
  4. Mathayo Chapter 24
  5. 2 Petro Chapter 1
  6. Luka Chapter 4
  7. Mathayo Chapter 27

Related Chapters & Readings

  1. Mambo ya Walawi Chapter 5
  2. 2 Wakorintho Chapter 9
  3. 2 Yohana Chapter 1
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 24
  5. Kutoka Chapter 17
  6. Matendo ya Mitume Chapter 18
  7. 2 Samweli Chapter 24
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *