Read Ufunuo wa Yohana Chapter 20 Online
Read Ufunuo wa Yohana Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ufunuo wa Yohana and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ufunuo wa Yohana 20
Sura 20
1. Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3. akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
4. Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6. Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
7. Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8. naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
10. Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
11. Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14. Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
About Ufunuo wa Yohana Chapter 20
Read Ufunuo wa Yohana Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ufunuo wa Yohana
Chapter: 20
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ufunuo wa Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ufunuo wa Yohana Chapter 20 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ufunuo wa Yohana Chapter 20?
Ufunuo wa Yohana Chapter 20 is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ufunuo wa Yohana Chapter 20 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 3
- Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 2
- Waebrania Chapter 12
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 8
Explore More from ufunuo-wa-yohana
- Ufunuo wa Yohana Chapter 16
- Ufunuo wa Yohana Chapter 8
- Ufunuo wa Yohana Chapter 6
- Ufunuo wa Yohana Chapter 1
- Ufunuo wa Yohana Chapter 18
- Ufunuo wa Yohana Chapter 19
- Ufunuo wa Yohana Chapter 11