Ufunuo wa Yohana Chapter 3

For English

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 3 Online

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ufunuo wa Yohana and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Ufunuo wa Yohana 3

Sura 3

1. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

2. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

3. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.

4. Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

5. Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

6. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

7. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

8. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

9. Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

10. Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

11. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

12. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

13. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

14. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

About Ufunuo wa Yohana Chapter 3

Read Ufunuo wa Yohana Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Ufunuo wa Yohana
Chapter: 3
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ufunuo wa Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Ufunuo wa Yohana Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Ufunuo wa Yohana Chapter 3?

Ufunuo wa Yohana Chapter 3 is part of the Book of Ufunuo wa Yohana in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Ufunuo wa Yohana Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 3
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 2
  4. Yohana Chapter 1
  5. Waebrania Chapter 12
  6. Waebrania Chapter 6
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 8

Explore More from ufunuo-wa-yohana

  1. Ufunuo wa Yohana Chapter 6
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 19
  3. Ufunuo wa Yohana Chapter 20
  4. Ufunuo wa Yohana Chapter 5
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 22
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 18
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 21

Related Chapters & Readings

  1. Nehemia Chapter 4
  2. Isaya Chapter 60
  3. 2 Samweli Chapter 13
  4. 2 Wafalme Chapter 25
  5. 1 Samweli Chapter 23
  6. Yoshua Chapter 2
  7. Tito Chapter 2
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *