Read Mathayo Chapter 4 Online
Read Mathayo Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mathayo in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mathayo and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Mathayo 4
Sura 4
1. Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
2. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
3. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
4. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
5. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6. akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9. akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
11. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
12. Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;
13. akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
14. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
15. Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa,
16. Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.
17. Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
18. Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
19. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
20. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
22. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.
23. Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.
24. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
25. Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani
About Mathayo Chapter 4
Read Mathayo Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mathayo in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Mathayo
Chapter: 4
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mathayo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Mathayo Chapter 4 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Mathayo Chapter 4?
Mathayo Chapter 4 is part of the Book of Mathayo in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Mathayo Chapter 4 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 5
- Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 12
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 2
- Ufunuo wa Yohana Chapter 8
Explore More from mathayo
- Mathayo Chapter 24
- Mathayo Chapter 26
- Mathayo Chapter 5
- Mathayo Chapter 3
- Mathayo Chapter 10
- Mathayo Chapter 18
- Mathayo Chapter 6