Read Yakobo Chapter 1 Online
Read Yakobo Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yakobo in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yakobo and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Yakobo 1
Sura 1
1. Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.
2. Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3. mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
4. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
5. Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
9. Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;
10. bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.
11. Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.
12. Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.
13. Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
16. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.
17. Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
18. Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.
19. Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
20. kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.
21. Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
22. Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
23. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
26. Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
About Yakobo Chapter 1
Read Yakobo Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yakobo in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Yakobo
Chapter: 1
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yakobo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Yakobo Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Yakobo Chapter 1?
Yakobo Chapter 1 is part of the Book of Yakobo in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Yakobo Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 3
- Ufunuo wa Yohana Chapter 15
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 2
Explore More from yakobo
- Yakobo Chapter 4
- Yakobo Chapter 5
- Yakobo Chapter 1
- Yakobo Chapter 5
- Yakobo Chapter 2
- Yakobo Chapter 4
- Yakobo Chapter 2