1 Wakorintho Chapter 1

For English

Read 1 Wakorintho Chapter 1 Online

Read 1 Wakorintho Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wakorintho and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Wakorintho 1

Sura 1

1. Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,

2. kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.

3. Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.

4. Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;

5. kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;

6. kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu;

7. hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;

8. ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

9. Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.

10. Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.

11. Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.

12. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.

13. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

14. Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo;

15. mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu.

16. Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine.

17. Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.

18. Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

19. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa.

20. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

21. Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.

22. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;

23. bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;

24. bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.

25. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

26. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

27. bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

28. tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;

29. mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.

30. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;

31. kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

About 1 Wakorintho Chapter 1

Read 1 Wakorintho Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Wakorintho
Chapter: 1
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Wakorintho Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Wakorintho Chapter 1?

1 Wakorintho Chapter 1 is part of the Book of 1 Wakorintho in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Wakorintho Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-wakorintho

  1. 1 Wakorintho Chapter 14
  2. 1 Wakorintho Chapter 5
  3. 1 Wakorintho Chapter 2
  4. 1 Wakorintho Chapter 16
  5. 1 Wakorintho Chapter 13
  6. 1 Wakorintho Chapter 11
  7. 1 Wakorintho Chapter 8

Explore More from Agano Jipya

  1. Luka Chapter 10
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 11
  3. Matendo ya Mitume Chapter 28
  4. Wagalatia Chapter 1
  5. Waefeso Chapter 5
  6. Mathayo Chapter 22
  7. 1 Wakorintho Chapter 5

Related Chapters & Readings

  1. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 13
  2. Zaburi Chapter 67
  3. Kutoka Chapter 8
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  5. Ayubu Chapter 10
  6. Mwanzo Chapter 49
  7. Yohana Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *