Read Yakobo Chapter 3 Online
Read Yakobo Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yakobo in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yakobo and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Yakobo 3
Sura 3
1. Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
2. Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
3. Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.
4. Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
5. Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6. Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
7. Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8. Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9. Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12. Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.
13. N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.
14. Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
15. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.
16. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
17. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
18. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
About Yakobo Chapter 3
Read Yakobo Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yakobo in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Yakobo
Chapter: 3
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yakobo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Yakobo Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Yakobo Chapter 3?
Yakobo Chapter 3 is part of the Book of Yakobo in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Yakobo Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 3
- Ufunuo wa Yohana Chapter 15
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 2
Explore More from yakobo
- Yakobo Chapter 4
- Yakobo Chapter 2
- Yakobo Chapter 5
- Yakobo Chapter 5
- Yakobo Chapter 3
- Yakobo Chapter 1
- Yakobo Chapter 2