Read Warumi Chapter 12 Online
Read Warumi Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Warumi in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Warumi and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Warumi 12
Sura 12
1. Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3. Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
4. Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
5. Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
6. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7. ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8. mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
9. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
10. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11. kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12. kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
13. kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
16. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
17. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
About Warumi Chapter 12
Read Warumi Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Warumi in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Warumi
Chapter: 12
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Warumi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Warumi Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Warumi Chapter 12?
Warumi Chapter 12 is part of the Book of Warumi in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Warumi Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Ufunuo wa Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 11
- Waebrania Chapter 10
Explore More from warumi
- Warumi Chapter 3
- Warumi Chapter 4
- Warumi Chapter 11
- Warumi Chapter 5
- Warumi Chapter 16
- Warumi Chapter 1
- Warumi Chapter 10