Read Mithali Chapter 6 Online
Read Mithali Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mithali and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Mithali 6
Sura 6
1. Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono,
2. Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
3. Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako.
4. Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia.
5. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.
6. Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu,
8. Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?
10. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
11. Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
12. Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.
13. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake.
14. Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.
15. Basi msiba utampata kwa ghafula; Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.
16. Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18. Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19. Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
20. Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.
21. Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.
22. Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.
23. Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
24. Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
25. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
26. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani
27. Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?
28. Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?
29. Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
30. Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;
31. Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.
32. Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
33. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
34. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.
35. Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
About Mithali Chapter 6
Read Mithali Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Mithali
Chapter: 6
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mithali. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Mithali Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Mithali Chapter 6?
Mithali Chapter 6 is part of the Book of Mithali in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Mithali Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
Explore More from mithali
- Mithali Chapter 25
- Mithali Chapter 23
- Mithali Chapter 2
- Mithali Chapter 1
- Mithali Chapter 17
- Mithali Chapter 3
- Mithali Chapter 20