1 Petro Chapter 4

For English

Read 1 Petro Chapter 4 Online

Read 1 Petro Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Petro and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Petro 4

Sura 4

1. Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.

2. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.

3. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

4. mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.

5. Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.

6. Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.

7. Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.

8. Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

9. Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika;

10. kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.

11. Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

12. Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.

13. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

14. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.

15. Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.

16. Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.

17. Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?

18. Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?

19. Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.

About 1 Petro Chapter 4

Read 1 Petro Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Petro
Chapter: 4
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Petro. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Petro Chapter 4 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Petro Chapter 4?

1 Petro Chapter 4 is part of the Book of 1 Petro in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Petro Chapter 4 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-petro

  1. 1 Petro Chapter 2
  2. 1 Petro Chapter 1
  3. 1 Petro Chapter 5
  4. 1 Petro Chapter 3

Explore More from Agano Jipya

  1. Warumi Chapter 6
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 12
  3. 1 Wakorintho Chapter 5
  4. 1 Wakorintho Chapter 16
  5. Matendo ya Mitume Chapter 13
  6. 1 Wakorintho Chapter 8
  7. 2 Timotheo Chapter 3

Related Chapters & Readings

  1. Wimbo Ulio Bora Chapter 3
  2. Yeremia Chapter 29
  3. Kutoka Chapter 9
  4. Marko Chapter 1
  5. Ayubu Chapter 25
  6. Matendo ya Mitume Chapter 6
  7. Zaburi Chapter 110
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *