Read 2 Wakorintho Chapter 6 Online
Read 2 Wakorintho Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wakorintho and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Wakorintho 6
Sura 6
1. Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
2. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)
3. Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;
4. bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;
5. katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;
6. katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;
7. katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
8. kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli;
9. kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;
10. kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
11. Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa.
12. Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu.
13. Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.
14. Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15. Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16. Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
About 2 Wakorintho Chapter 6
Read 2 Wakorintho Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Wakorintho
Chapter: 6
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Wakorintho Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Wakorintho Chapter 6?
2 Wakorintho Chapter 6 is part of the Book of 2 Wakorintho in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Wakorintho Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2-wakorintho
- 2 Wakorintho Chapter 12
- 2 Wakorintho Chapter 8
- 2 Wakorintho Chapter 7
- 2 Wakorintho Chapter 13
- 2 Wakorintho Chapter 11
- 2 Wakorintho Chapter 10
- 2 Wakorintho Chapter 3
Explore More from Agano Jipya
- Mathayo Chapter 8
- Mathayo Chapter 11
- 1 Timotheo Chapter 2
- Mathayo Chapter 26
- 1 Yohana Chapter 3
- Marko Chapter 16
- 2 Yohana Chapter 1