Yeremia Chapter 16

For English

Read Yeremia Chapter 16 Online

Read Yeremia Chapter 16 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yeremia in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yeremia and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Yeremia 16

Sura 16

1. Tena neno la Bwana likanijia, kusema,

2. Wewe hutaoa mke, wala hutakuwa na wana wala binti mahali hapa.

3. Maana Bwana asema hivi, katika habari za wana, na katika habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na katika habari za mama zao waliowazaa, na katika habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;

4. watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.

5. Maana Bwana asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema Bwana, hata fadhili zangu na rehema zangu.

6. Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikata-kata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;

7. wala watu hawatamega mkate kwa ajili yao, wakati wa kuomboleza, ili kuwafariji kwa ajili yao waliokufa; wala watu hawatawapa kikombe cha faraja, wanywe kwa ajili ya baba yao au mama yao.

8. Wala usiingie ndani katika nyumba yenye karamu, kuketi pamoja nao, na kula na kunywa.

9. Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi, mbele ya macho yenu, na katika siku zenu, nitaikomesha sauti ya furaha, na sauti ya kicheko, mahali hapa; sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi.

10. Tena itakuwa, utakapowaonyesha watu hawa maneno haya yote, nao wakakuambia, Mbona Bwana amenena juu yetu mabaya haya makuu? Uovu wetu ni uovu gani? Na dhambi yetu, tuliyomtenda Bwana, Mungu wetu, ni nini?

11. Ndipo utakapowaambia, Ni kwa sababu baba zenu wameniacha mimi, asema Bwana, na kuwafuata miungu mingine, na kuwatumikia, na kuwaabudu, wakaniacha mimi, wasiishike torati yangu;

12. na ninyi mmetenda mabaya kupita baba zenu; maana angalieni, mnaenenda kila mmoja wenu kwa ushupavu wa moyo wake mbaya, msinisikilize mimi;

13. basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.

14. Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya Misri;

15. lakini, Aishivyo Bwana, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi zote alikowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.

16. Tazama, asema Bwana, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.

17. Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.

18. Nami kwanza nitawalipa uovu wao na dhambi zao maradufu, kwa kuwa wameitia unajisi nchi yangu, kwa mizoga ya vitu vyao vichukizavyo, na kuujaza urithi wangu kwa machukizo yao.

19. Ee Bwana, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.

20. Je! Mwanadamu ajifanyie miungu, wasio miungu?

21. Basi, tazama, nitawajulisha, mara moja hii nitawajulisha, mkono wangu, na nguvu zangu; nao watajua ya kuwa, jina langu ni YEHOVA.

About Yeremia Chapter 16

Read Yeremia Chapter 16 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yeremia in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Yeremia
Chapter: 16
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yeremia. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Yeremia Chapter 16 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Yeremia Chapter 16?

Yeremia Chapter 16 is part of the Book of Yeremia in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Yeremia Chapter 16 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 14
  7. Isaya Chapter 5

Explore More from Yeremia

  1. Yeremia Chapter 31
  2. Yeremia Chapter 9
  3. Yeremia Chapter 11
  4. Yeremia Chapter 21
  5. Yeremia Chapter 46
  6. Yeremia Chapter 41
  7. Yeremia Chapter 44

Related Chapters & Readings

  1. 1 Samweli Chapter 11
  2. Mathayo Chapter 17
  3. Yohana Chapter 16
  4. Zaburi Chapter 138
  5. Wagalatia Chapter 2
  6. 1 Samweli Chapter 12
  7. Hesabu Chapter 7
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *