Read Wakolosai Chapter 4 Online
Read Wakolosai Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wakolosai in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Wakolosai and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Wakolosai 4
Sura 4
1. Ninyi akina bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
2. Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
3. mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
4. ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.
5. Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
6. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
7. Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;
8. ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu;
9. pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.
10. Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
11. Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.
12. Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.
13. Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli.
14. Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.
15. Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
16. Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
17. Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.
18. Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.
About Wakolosai Chapter 4
Read Wakolosai Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wakolosai in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Wakolosai
Chapter: 4
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Wakolosai. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Wakolosai Chapter 4 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Wakolosai Chapter 4?
Wakolosai Chapter 4 is part of the Book of Wakolosai in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Wakolosai Chapter 4 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 5
- Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 12
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 2
- Ufunuo wa Yohana Chapter 8