Read Wakolosai Chapter 2 Online
Read Wakolosai Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wakolosai in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Wakolosai and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Wakolosai 2
Sura 2
1. Maana nataka ninyi mjue jinsi ilivyo kuu juhudi yangu niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili;
2. ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo;
3. ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.
4. Nasema neno hili, mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi.
5. Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.
6. Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;
7. wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.
8. Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
9. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
10. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.
11. Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
12. Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
13. Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;
14. akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
15. akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
16. Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17. mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
18. Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;
19. wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
20. Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
21. Msishike, msionje, msiguse;
22. (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
23. Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
About Wakolosai Chapter 2
Read Wakolosai Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wakolosai in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Wakolosai
Chapter: 2
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Wakolosai. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Wakolosai Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Wakolosai Chapter 2?
Wakolosai Chapter 2 is part of the Book of Wakolosai in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Wakolosai Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Ufunuo wa Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 11
- Waebrania Chapter 10