Read Matendo ya Mitume Chapter 20 Online
Read Matendo ya Mitume Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Matendo ya Mitume and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Matendo ya Mitume 20
Sura 20
1. Kishindo kile kilipokoma, Paulo akatuma kuwaita wanafunzi akawaonya, akaagana nao, kisha akaondoka aende zake mpaka Makedonia.
2. Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.
3. Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
4. Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.
5. Ila watu hao wamekwisha kutangulia wakamngojea Troa.
6. Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
7. Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
8. Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.
9. Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
10. Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
11. Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake.
12. Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.
13. Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu.
14. Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.
15. Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto.
16. Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.
17. Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.
18. Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote,
19. nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;
20. ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,
21. nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.
22. Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
23. isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.
24. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
25. Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.
26. Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote.
27. Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.
28. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
29. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
30. tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
31. Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.
32. Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.
33. Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.
34. Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.
35. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
36. Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote.
37. Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu,
38. wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.
About Matendo ya Mitume Chapter 20
Read Matendo ya Mitume Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Matendo ya Mitume
Chapter: 20
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Matendo ya Mitume. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Matendo ya Mitume Chapter 20 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Matendo ya Mitume Chapter 20?
Matendo ya Mitume Chapter 20 is part of the Book of Matendo ya Mitume in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Matendo ya Mitume Chapter 20 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 3
- Ufunuo wa Yohana Chapter 15
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 2
Explore More from matendo-ya-mitume
- Matendo ya Mitume Chapter 7
- Matendo ya Mitume Chapter 25
- Matendo ya Mitume Chapter 9
- Matendo ya Mitume Chapter 21
- Matendo ya Mitume Chapter 8
- Matendo ya Mitume Chapter 10
- Matendo ya Mitume Chapter 4