Read Mithali Chapter 25 Online
Read Mithali Chapter 25 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mithali and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Mithali 25
Sura 25
1. Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili.
2. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo.
3. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki.
4. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
5. Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki.
6. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu;
7. Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho,
8. Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.
9. Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine;
10. Yeye asikiaye asije akakutukana; Na aibu yako isiondoke.
11. Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha.
12. Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
13. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.
14. Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.
15. Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.
16. Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika.
17. Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
18. Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.
19. Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.
20. Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.
21. Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;
22. Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu.
23. Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
24. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
25. Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu, Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
26. Mwenye haki amwangukiapo mtu mbaya Ni kama chemchemi iliyochafuka, Na kisima kilichokanyagwa.
27. Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.
28. Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.
About Mithali Chapter 25
Read Mithali Chapter 25 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Mithali
Chapter: 25
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mithali. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Mithali Chapter 25 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Mithali Chapter 25?
Mithali Chapter 25 is part of the Book of Mithali in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Mithali Chapter 25 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from mithali
- Mithali Chapter 26
- Mithali Chapter 18
- Mithali Chapter 15
- Mithali Chapter 2
- Mithali Chapter 14
- Mithali Chapter 6
- Mithali Chapter 7