Read 2 Yohana Chapter 1 Online
Read 2 Yohana Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Yohana in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Yohana and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Yohana 1
Sura 1
1. Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
2. kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.
3. Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4. Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
5. Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
6. Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
7. Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
8. Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.
9. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
10. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11. Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.
12. Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.
13. Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.
About 2 Yohana Chapter 1
Read 2 Yohana Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Yohana in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Yohana
Chapter: 1
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Yohana. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Yohana Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Yohana Chapter 1?
2 Yohana Chapter 1 is part of the Book of 2 Yohana in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Yohana Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2 Yohana
Explore More from Agano Jipya
- Wafilipi Chapter 3
- 2 Petro Chapter 1
- Waebrania Chapter 13
- Matendo ya Mitume Chapter 21
- Matendo ya Mitume Chapter 7
- Mathayo Chapter 6
- Mathayo Chapter 8