Read 1 Wakorintho Chapter 6 Online
Read 1 Wakorintho Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wakorintho and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
1 Wakorintho 6
Sura 6
1. Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
2. Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
3. Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
4. Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?
5. Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?
6. Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini.
7. Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang'anywa mali zenu?
8. Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang'anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
9. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10. wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
11. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
12. Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
13. Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
14. Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.
15. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16. Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
17. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
18. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20. maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
About 1 Wakorintho Chapter 6
Read 1 Wakorintho Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 1 Wakorintho
Chapter: 6
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 1 Wakorintho Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 1 Wakorintho Chapter 6?
1 Wakorintho Chapter 6 is part of the Book of 1 Wakorintho in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 1 Wakorintho Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 1-wakorintho
- 1 Wakorintho Chapter 14
- 1 Wakorintho Chapter 5
- 1 Wakorintho Chapter 2
- 1 Wakorintho Chapter 11
- 1 Wakorintho Chapter 8
- 1 Wakorintho Chapter 1
- 1 Wakorintho Chapter 16
Explore More from Agano Jipya
- Luka Chapter 5
- Luka Chapter 20
- Ufunuo wa Yohana Chapter 11
- Marko Chapter 14
- Yohana Chapter 10
- Yohana Chapter 3
- Yohana Chapter 15