Mwanzo Chapter 17

For English

Read Mwanzo Chapter 17 Online

Read Mwanzo Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

A+ A A-

Mwanzo 17

Sura 17

1. Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.

2. Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.

3. Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,

4. Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,

5. wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.

6. Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.

7. Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

8. Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.

9. Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.

10. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

11. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.

12. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.

13. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.

14. Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.

15. Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.

16. Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.

17. Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?

18. Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

19. Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

20. Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

21. Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.

22. Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.

23. Ibrahimu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.

24. Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake.

25. Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.

26. Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe.

27. Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.

About Mwanzo Chapter 17

Read Mwanzo Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mwanzo
Chapter: 17
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mwanzo Chapter 17 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mwanzo Chapter 17?

Mwanzo Chapter 17 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 17 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from mwanzo

  1. Mwanzo Chapter 33
  2. Mwanzo Chapter 38
  3. Mwanzo Chapter 31
  4. Mwanzo Chapter 20
  5. Mwanzo Chapter 46
  6. Mwanzo Chapter 45
  7. Mwanzo Chapter 8

Related Chapters & Readings

  1. Mithali Chapter 13
  2. Sefania Chapter 2
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  4. Mwanzo Chapter 3
  5. Mithali Chapter 26
  6. Isaya Chapter 33
  7. 1 Wafalme Chapter 19
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *