Mwanzo Chapter 21

For English

Read Mwanzo Chapter 21 Online

Read Mwanzo Chapter 21 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mwanzo 21

Sura 21

1. Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema.

2. Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

3. Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.

4. Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.

5. Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka.

6. Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.

7. Akasema, N'nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.

8. Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.

9. Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.

10. Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.

11. Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.

12. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

13. Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.

14. Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.

15. Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.

16. Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.

17. Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.

18. Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.

19. Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.

20. Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.

21. Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

22. Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.

23. Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.

24. Ibrahimu akasema, Nitaapa.

25. Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumwa wa Abimeleki wamekinyang'anya.

26. Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.

27. Ibrahimu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.

28. Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao.

29. Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?

30. Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.

31. Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.

32. Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

33. Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele.

34. Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

About Mwanzo Chapter 21

Read Mwanzo Chapter 21 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mwanzo
Chapter: 21
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mwanzo Chapter 21 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mwanzo Chapter 21?

Mwanzo Chapter 21 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 21 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 6
  3. Isaya Chapter 2
  4. Isaya Chapter 14
  5. Isaya Chapter 3
  6. Isaya Chapter 7
  7. Isaya Chapter 16

Explore More from mwanzo

  1. Mwanzo Chapter 7
  2. Mwanzo Chapter 50
  3. Mwanzo Chapter 35
  4. Mwanzo Chapter 15
  5. Mwanzo Chapter 17
  6. Mwanzo Chapter 43
  7. Mwanzo Chapter 48

Related Chapters & Readings

  1. Mithali Chapter 21
  2. Yohana Chapter 3
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Yohana Chapter 11
  5. Zaburi Chapter 147
  6. Waamuzi Chapter 3
  7. Ayubu Chapter 39
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *