Mwanzo Chapter 13

For English

Read Mwanzo Chapter 13 Online

Read Mwanzo Chapter 13 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mwanzo 13

Sura 13

1. Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini.

2. Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.

3. Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza kati ya Betheli na Ai;

4. napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la Bwana hapo.

5. Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.

6. Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.

7. Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.

8. Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.

9. Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.

10. Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.

11. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao.

12. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma.

13. Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.

14. Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;

15. maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

16. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika.

17. Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.

18. Basi Abramu akajongeza hema yake, akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.

About Mwanzo Chapter 13

Read Mwanzo Chapter 13 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mwanzo
Chapter: 13
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mwanzo Chapter 13 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mwanzo Chapter 13?

Mwanzo Chapter 13 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 13 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from mwanzo

  1. Mwanzo Chapter 12
  2. Mwanzo Chapter 17
  3. Mwanzo Chapter 37
  4. Mwanzo Chapter 26
  5. Mwanzo Chapter 35
  6. Mwanzo Chapter 32
  7. Mwanzo Chapter 48

Related Chapters & Readings

  1. 1 Timotheo Chapter 5
  2. Yoshua Chapter 15
  3. 2 Wakorintho Chapter 5
  4. Hosea Chapter 11
  5. Zaburi Chapter 104
  6. Zaburi Chapter 120
  7. 1 Wafalme Chapter 19
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *