Read Mwanzo Chapter 7 Online
Read Mwanzo Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Mwanzo 7
Sura 7
1. Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
2. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke.
3. Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.
4. Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
5. Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.
6. Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.
7. Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika.
8. Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi,
9. wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
10. Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi.
11. Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
12. Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku.
13. Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye;
14. wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote.
15. Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.
16. Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; Bwana akamfungia.
17. Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi.
18. Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji.
19. Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa.
20. Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.
21. Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;
22. kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.
23. Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.
24. Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
About Mwanzo Chapter 7
Read Mwanzo Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Mwanzo
Chapter: 7
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Mwanzo Chapter 7 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Mwanzo Chapter 7?
Mwanzo Chapter 7 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 7 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from mwanzo
- Mwanzo Chapter 44
- Mwanzo Chapter 2
- Mwanzo Chapter 25
- Mwanzo Chapter 31
- Mwanzo Chapter 30
- Mwanzo Chapter 28
- Mwanzo Chapter 24