Zekaria Chapter 7

For English

Read Zekaria Chapter 7 Online

Read Zekaria Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zekaria and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zekaria 7

Sura 7

1. Ikawa katika mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi wa kenda, yaani, Kisleu.

2. Basi watu wa Betheli walikuwa wamewatuma Shareza na Regem-meleki, na watu wao, ili kuomba fadhili za Bwana,

3. na kusema na makuhani wa nyumba ya Bwana wa majeshi, na hao manabii, ya kwamba, Je! Yanipasa kulia katika mwezi wa tano, na kujitenga na watu, kama nilivyofanya miaka hii mingi iliyopita?

4. Ndipo neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema,

5. Waambie watu wote wa nchi, na hao makuhani, ukisema, Hapo mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na mwezi wa saba, katika miaka hiyo sabini, je! Mlinifungia mimi kwa lo lote; mlinifungia mimi?

6. Na wakati mlapo chakula na kunywa, je! Hamli kwa ajili ya nafsi zenu, na kunywa kwa ajili ya nafsi zenu?

7. Je! Hayo siyo maneno aliyoyasema Bwana kwa vinywa vya manabii wa zamani, wakati Yerusalemu ulipokaliwa na watu na kufanikiwa, na miji yake iliyokuwa ikiuzunguka; na wakati ule ambao nchi ya Negebu na Shefela ilipokuwa ikikaliwa na watu?

8. Kisha neno la Bwana likamjia Zekaria, kusema,

9. Bwana wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;

10. tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake.

11. Lakini hao walikataa kusikiliza, wakageuza bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie.

12. Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na maneno ya Bwana wa majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa kwanza; kwa sababu hiyo ghadhabu kuu ikatoka kwa Bwana wa majeshi.

13. Ikawa kwa sababu alilia, wao wasitake kusikiliza; basi, wao nao watalia, wala mimi sitasikiliza, asema Bwana wa majeshi.

14. Lakini nitawatawanya kwa upepo wa kisulisuli, katikati ya mataifa yote wasiowajua. Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa ukiwa nchi baada yao, hata hapakuwa na mtu aliyepita kati yake, wala aliyerudi; maana waliifanya nchi iliyopendeza sana kuwa ukiwa.

About Zekaria Chapter 7

Read Zekaria Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zekaria
Chapter: 7
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zekaria. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zekaria Chapter 7 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zekaria Chapter 7?

Zekaria Chapter 7 is part of the Book of Zekaria in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zekaria Chapter 7 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from zekaria

  1. Zekaria Chapter 1
  2. Zekaria Chapter 11
  3. Zekaria Chapter 4
  4. Zekaria Chapter 10
  5. Zekaria Chapter 14
  6. Zekaria Chapter 2
  7. Zekaria Chapter 12

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 13
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 32
  3. 2 Timotheo Chapter 2
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 20
  5. Matendo ya Mitume Chapter 5
  6. Zaburi Chapter 61
  7. Amosi Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *