Mwanzo Chapter 8

For English

Read Mwanzo Chapter 8 Online

Read Mwanzo Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mwanzo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mwanzo 8

Sura 8

1. Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;

2. chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;

3. maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka.

4. Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.

5. Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.

6. Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;

7. akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.

8. Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;

9. bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.

10. Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,

11. njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.

12. Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.

13. Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.

14. Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.

15. Mungu akamwambia Nuhu, akisema,

16. Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe.

17. Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.

18. Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;

19. kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.

20. Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

21. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.

22. Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.

About Mwanzo Chapter 8

Read Mwanzo Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mwanzo in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mwanzo
Chapter: 8
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mwanzo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mwanzo Chapter 8 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mwanzo Chapter 8?

Mwanzo Chapter 8 is part of the Book of Mwanzo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mwanzo Chapter 8 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from mwanzo

  1. Mwanzo Chapter 27
  2. Mwanzo Chapter 14
  3. Mwanzo Chapter 41
  4. Mwanzo Chapter 30
  5. Mwanzo Chapter 6
  6. Mwanzo Chapter 25
  7. Mwanzo Chapter 23

Related Chapters & Readings

  1. Kutoka Chapter 13
  2. 1 Wafalme Chapter 18
  3. Kumbukumbu la Torati Chapter 13
  4. Warumi Chapter 11
  5. Zaburi Chapter 98
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 5
  7. Hosea Chapter 10
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *