1 Samweli Chapter 29

For English

Read 1 Samweli Chapter 29 Online

Read 1 Samweli Chapter 29 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Samweli and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Samweli 29

Sura 29

1. Basi hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki; nao Waisraeli wakafanya kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.

2. Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.

3. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakasema, Waebrania hawa wafanyani hapa? Naye Akishi akawaambia wakuu wa Wafilisti, Je! Siye huyu Daudi, yule mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amefuatana na mimi siku hizi, naam, miaka hii, wala mimi nisione hatia kwake, tangu hapo aliponiangukia mimi hata leo?

4. Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?

5. Je! Siye huyo Daudi, ambaye waliimbiana habari zake katika michezo, wakisema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake?

6. Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo Bwana, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.

7. Basi sasa urudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao mashehe wa Wafilisti.

8. Naye Daudi akamwambia Akishi, Lakini mimi nimefanyaje? Nawe umeona nini kwangu mimi mtumwa wako, muda wote niliokaa mbele yako hata leo, nisipate ruhusa niende na kupigana na adui za bwana wangu mfalme?

9. Akishi akajibu, akamwambia Daudi, Mimi najua ya kuwa u mwema machoni pangu, kama malaika wa Mungu; ila hao wakuu wa Wafilisti wamesema, Huyu hatakwea pamoja nasi kwenda vitani.

10. Kwa hiyo sasa amka asubuhi na mapema, wewe na watumwa wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; nanyi mtakapoamka asubuhi na mapema, na kupata mwanga, nendeni zenu.

11. Basi Daudi akaamka asubuhi na mapema, yeye na watu wake, kwenda zao asubuhi, kuirudia nchi ya Wafilisti. Nao Wafilisti wakakwea kwenda Yezreeli.

About 1 Samweli Chapter 29

Read 1 Samweli Chapter 29 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Samweli
Chapter: 29
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Samweli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Samweli Chapter 29 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Samweli Chapter 29?

1 Samweli Chapter 29 is part of the Book of 1 Samweli in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Samweli Chapter 29 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-samweli

  1. 1 Samweli Chapter 1
  2. 1 Samweli Chapter 11
  3. 1 Samweli Chapter 2
  4. 1 Samweli Chapter 6
  5. 1 Samweli Chapter 23
  6. 1 Samweli Chapter 22
  7. 1 Samweli Chapter 9

Explore More from Agano la Kale

  1. Mwanzo Chapter 36
  2. Zaburi Chapter 36
  3. Yoshua Chapter 3
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 9
  5. Mambo ya Walawi Chapter 25
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 7
  7. Wimbo Ulio Bora Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. Ezra Chapter 1
  2. Yeremia Chapter 6
  3. 2 Wafalme Chapter 10
  4. Waefeso Chapter 1
  5. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8
  6. Ayubu Chapter 41
  7. Waebrania Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *