Mithali Chapter 12

For English

Read Mithali Chapter 12 Online

Read Mithali Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mithali and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mithali 12

Sura 12

1. Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.

2. Mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwana; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye.

3. Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu; Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe.

4. Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.

5. Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.

6. Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.

7. Waovu huangamia, hata hawako tena; Bali nyumba ya mwenye haki itasimama.

8. Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.

9. Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa, Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.

10. Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.

11. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu.

12. Asiye haki hutamani nyavu za wabaya; Bali shina lao wenye haki huleta matunda.

13. Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu.

14. Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake; Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.

15. Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.

16. Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.

17. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.

18. Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.

19. Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.

20. Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.

21. Mwenye haki hatapatikana na msiba wo wote; Bali wasio haki watajazwa mabaya.

22. Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.

23. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.

24. Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.

25. Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha; Bali neno jema huufurahisha.

26. Mwenye haki ni kiongozi cha mwenzake; Bali njia ya wasio haki huwakosesha.

27. Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.

28. Katika njia ya haki kuna uhai; Wala hakuna mauti katika mapito yake.

About Mithali Chapter 12

Read Mithali Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mithali in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mithali
Chapter: 12
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mithali. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mithali Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mithali Chapter 12?

Mithali Chapter 12 is part of the Book of Mithali in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mithali Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 5
  6. Isaya Chapter 7
  7. Isaya Chapter 16

Explore More from mithali

  1. Mithali Chapter 17
  2. Mithali Chapter 23
  3. Mithali Chapter 29
  4. Mithali Chapter 10
  5. Mithali Chapter 7
  6. Mithali Chapter 18
  7. Mithali Chapter 24

Related Chapters & Readings

  1. Luka Chapter 24
  2. 1 Wafalme Chapter 20
  3. Yeremia Chapter 12
  4. Ayubu Chapter 20
  5. Mambo ya Walawi Chapter 4
  6. 2 Timotheo Chapter 3
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 19
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *