Kutoka Chapter 40

For English

Read Kutoka Chapter 40 Online

Read Kutoka Chapter 40 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kutoka and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kutoka 40

Sura 40

1. Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2. Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.

3. Nawe utatia ndani yake sanduku la ushuhuda, nawe utalisitiri hilo sanduku kwa pazia.

4. Nawe utaleta meza na kuitia ndani, na kuviweka sawasawa vile vitu juu yake; kisha utakileta ndani kile kinara cha taa, na kuziwasha taa zake.

5. Kisha utaisimamisha madhabahu ya dhahabu kwa kufukizia uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na kulitia pazia mlangoni mwa hiyo maskani.

6. Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.

7. Kisha utaliweka birika kati ya hema ya kukutania na hiyo madhabahu, nawe utatia maji ndani yake.

8. Kisha utausimamisha ukuta wa ua kuuzunguka pande zote, na kuitundika sitara ya lango la ua.

9. Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.

10. Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana.

11. Kisha utalitia mafuta birika na tako lake, na kuliweka liwe takatifu.

12. Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.

13. Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

14. Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;

15. nawe utawatia mafuta kama ulivyomtia mafuta baba yao, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani; na huko kutiwa mafuta kwao kutakuwa ni kwa ukuhani wa milele katika vizazi vyao vyote.

16. Musa akafanya hayo yote; kama yote Bwana aliyoagiza ndivyo alivyofanya.

17. Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi ile maskani ilisimamishwa.

18. Musa akaisimamisha maskani, akayaweka matako yake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake.

19. Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

20. Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku;

21. kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

22. Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia.

23. Akaipanga ile mikate juu yake mbele za Bwana; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

24. Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.

25. Kisha akaziwasha taa zake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwamuru Musa.

26. Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.

27. Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama Bwana alivyomwamuru Musa.

28. Akalitia pazia la mlango wa maskani.

29. Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

30. Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.

31. Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake;

32. hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama Bwana alivyomwamuru Musa.

33. Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

34. Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.

35. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.

36. Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,

37. bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena.

38. Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.

About Kutoka Chapter 40

Read Kutoka Chapter 40 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kutoka
Chapter: 40
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kutoka. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kutoka Chapter 40 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kutoka Chapter 40?

Kutoka Chapter 40 is part of the Book of Kutoka in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kutoka Chapter 40 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 5
  6. Isaya Chapter 7
  7. Isaya Chapter 16

Explore More from Kutoka

  1. Kutoka Chapter 10
  2. Kutoka Chapter 17
  3. Kutoka Chapter 27
  4. Kutoka Chapter 21
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 5
  7. Kutoka Chapter 18

Related Chapters & Readings

  1. Mhubiri Chapter 12
  2. Ezekieli Chapter 23
  3. Marko Chapter 7
  4. Matendo ya Mitume Chapter 5
  5. Yohana Chapter 2
  6. 1 Samweli Chapter 27
  7. Kutoka Chapter 24
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *