2 Mambo ya Nyakati Chapter 5

For English

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 Online

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

A+ A A-

2 Mambo ya Nyakati 5

Sura 5

1. Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.

2. Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

3. Wakakutana watu wote wa Israeli mbele ya mfalme wakati wa sikukuu, katika mwezi wa saba.

4. Wakaja wazee wote wa Israeli, nao Walawi wakajitwika sanduku.

5. Wakalipandisha sanduku, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani, vitu hivyo makuhani Walawi wakavipandisha.

6. Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli, waliokutanika kwake, walikuwako mbele ya sanduku, wakichinja dhabihu za kondoo na ng'ombe, wasiohesabika wala kujumlishwa kwa kuwa wengi.

7. Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.

8. Kwa maana makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.

9. Na ile miti ilikuwa mirefu, hata ncha za miti zilionekana sandukuni mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo.

10. Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.

11. Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao;

12. tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;)

13. hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana,

14. hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.

About 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Mambo ya Nyakati
Chapter: 5
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5?

2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2 MambO Ya Nyakati

  1. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 21
  2. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  3. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 13
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 12
  5. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 4
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 35
  7. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 26

Explore More from Agano la Kale

  1. Yoshua Chapter 22
  2. Zaburi Chapter 42
  3. Waamuzi Chapter 20
  4. Yeremia Chapter 14
  5. Yeremia Chapter 4
  6. Mwanzo Chapter 43
  7. Mwanzo Chapter 40

Related Chapters & Readings

  1. 1 Samweli Chapter 29
  2. Zaburi Chapter 137
  3. Mambo ya Walawi Chapter 25
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 27
  5. Kutoka Chapter 4
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *