Read Matendo ya Mitume Chapter 9 Online
Read Matendo ya Mitume Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Matendo ya Mitume and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Matendo ya Mitume 9
Sura 9
1. Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu,
2. akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
3. Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.
4. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
5. Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
6. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.
7. Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.
8. Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
10. Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.
11. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
12. naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
13. Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
14. hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
15. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
16. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
17. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19. akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
20. Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
21. Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?
22. Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
23. Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue;
24. lakini hila yao ikajulikana na Sauli. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.
25. Wanafunzi wake wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu.
26. Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.
27. Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
28. Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka.
29. Akahubiri kwa jina la Bwana kwa ushujaa, akinena na kuhojiana na Wayahudi wa Kiyunani. Nao wakajaribu kumwua.
30. Lakini ndugu walipopata habari wakamchukua mpaka Kaisaria, wakampeleka aende Tarso.
31. Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
32. Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida.
33. Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.
34. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.
35. Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana.
36. Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
37. Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
38. Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.
39. Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
40. Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
41. Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.
42. Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana.
43. Basi Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.
About Matendo ya Mitume Chapter 9
Read Matendo ya Mitume Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Matendo ya Mitume
Chapter: 9
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Matendo ya Mitume. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Matendo ya Mitume Chapter 9 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Matendo ya Mitume Chapter 9?
Matendo ya Mitume Chapter 9 is part of the Book of Matendo ya Mitume in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Matendo ya Mitume Chapter 9 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Waebrania Chapter 3
- Waebrania Chapter 2
- Yohana Chapter 1
Explore More from matendo-ya-mitume
- Matendo ya Mitume Chapter 21
- Matendo ya Mitume Chapter 2
- Matendo ya Mitume Chapter 17
- Matendo ya Mitume Chapter 11
- Matendo ya Mitume Chapter 20
- Matendo ya Mitume Chapter 15
- Matendo ya Mitume Chapter 7