Matendo ya Mitume Chapter 28

For English

Read Matendo ya Mitume Chapter 28 Online

Read Matendo ya Mitume Chapter 28 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Matendo ya Mitume and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Matendo ya Mitume 28

Sura 28

1. Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita.

2. Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana waliwasha moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyonyesha na kwa sababu ya baridi.

3. Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi.

4. Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.

5. Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara.

6. Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.

7. Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkuu wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu.

8. Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na kumpoza.

9. Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakapozwa;

10. nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; basi tulipoabiri wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.

11. Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha.

12. Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu.

13. Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli.

14. Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.

15. Na kutoka huko ndugu, waliposikia habari zetu, wakaja kutulaki mpaka Soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akachangamka.

16. Tulipoingia Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.

17. Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu.

18. Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa.

19. Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.

20. Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.

21. Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako.

22. Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali.

23. Wakiisha kuagana naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni.

24. Wengine waliamini yale yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini.

25. Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,

26. akisema, Enenda kwa watu hawa, ukawaambie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona, mtaona wala hamtatambua;

27. Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.

28. Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!

29. Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao.]

30. Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea,

31. akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.

About Matendo ya Mitume Chapter 28

Read Matendo ya Mitume Chapter 28 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Matendo ya Mitume in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Matendo ya Mitume
Chapter: 28
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Matendo ya Mitume. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Matendo ya Mitume Chapter 28 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Matendo ya Mitume Chapter 28?

Matendo ya Mitume Chapter 28 is part of the Book of Matendo ya Mitume in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Matendo ya Mitume Chapter 28 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 3
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 15
  6. Waebrania Chapter 4
  7. Waebrania Chapter 2

Explore More from matendo-ya-mitume

  1. Matendo ya Mitume Chapter 5
  2. Matendo ya Mitume Chapter 19
  3. Matendo ya Mitume Chapter 25
  4. Matendo ya Mitume Chapter 21
  5. Matendo ya Mitume Chapter 2
  6. Matendo ya Mitume Chapter 26
  7. Matendo ya Mitume Chapter 11

Related Chapters & Readings

  1. Waamuzi Chapter 12
  2. Kutoka Chapter 7
  3. Ayubu Chapter 2
  4. Kutoka Chapter 39
  5. 1 Wakorintho Chapter 3
  6. 2 Wakorintho Chapter 13
  7. Warumi Chapter 3
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *