Read 2 Wakorintho Chapter 9 Online
Read 2 Wakorintho Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wakorintho and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Wakorintho 9
Sura 9
1. Kwa habari za kuwahudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.
2. Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa ajili yenu kwa Wamakedonia, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi wao.
3. Lakini naliwatuma hao ndugu, ili kujisifu kwetu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema;
4. kusudi, wakija Wamakedonia pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, (tusiseme ninyi), katika hali hiyo ya kutumaini.
5. Basi naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu.
6. Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
7. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
8. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
9. kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.
10. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
11. mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
12. Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
13. kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.
14. Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu.
15. Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
About 2 Wakorintho Chapter 9
Read 2 Wakorintho Chapter 9 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Wakorintho
Chapter: 9
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Wakorintho Chapter 9 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Wakorintho Chapter 9?
2 Wakorintho Chapter 9 is part of the Book of 2 Wakorintho in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Wakorintho Chapter 9 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2-wakorintho
- 2 Wakorintho Chapter 12
- 2 Wakorintho Chapter 8
- 2 Wakorintho Chapter 7
- 2 Wakorintho Chapter 13
- 2 Wakorintho Chapter 11
- 2 Wakorintho Chapter 10
- 2 Wakorintho Chapter 6
Explore More from Agano Jipya
- Yakobo Chapter 4
- Waebrania Chapter 12
- Waefeso Chapter 5
- Matendo ya Mitume Chapter 24
- 2 Timotheo Chapter 3
- Waebrania Chapter 13
- 3 Yohana Chapter 1