2 Timotheo Chapter 3

For English

Read 2 Timotheo Chapter 3 Online

Read 2 Timotheo Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Timotheo in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Timotheo and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

2 Timotheo 3

Sura 3

1. Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

2. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,

3. wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

4. wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;

5. wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

6. Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;

7. wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

8. Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

9. Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.

10. Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,

11. na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.

12. Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

13. lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.

14. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;

15. na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.

16. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

17. ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

About 2 Timotheo Chapter 3

Read 2 Timotheo Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Timotheo in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Timotheo
Chapter: 3
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Timotheo. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Timotheo Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Timotheo Chapter 3?

2 Timotheo Chapter 3 is part of the Book of 2 Timotheo in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Timotheo Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2-timotheo

  1. 2 Timotheo Chapter 1
  2. 2 Timotheo Chapter 2
  3. 2 Timotheo Chapter 4

Explore More from Agano Jipya

  1. 2 Wakorintho Chapter 8
  2. Mathayo Chapter 10
  3. Luka Chapter 12
  4. Yohana Chapter 18
  5. 2 Wakorintho Chapter 10
  6. Luka Chapter 4
  7. Waebrania Chapter 13

Related Chapters & Readings

  1. 1 Timotheo Chapter 4
  2. Ayubu Chapter 20
  3. Waamuzi Chapter 3
  4. 2 Wafalme Chapter 15
  5. Zaburi Chapter 60
  6. Isaya Chapter 48
  7. Matendo ya Mitume Chapter 11
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *