2 Wakorintho Chapter 12

For English

Read 2 Wakorintho Chapter 12 Online

Read 2 Wakorintho Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wakorintho and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

2 Wakorintho 12

Sura 12

1. Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.

2. Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.

3. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);

4. ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.

5. Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.

6. Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.

7. Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.

8. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.

9. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

10. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

11. Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.

12. Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.

13. Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.

14. Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.

15. Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?

16. Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.

17. Je! Mtu ye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu?

18. Nalimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?

19. Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.

20. Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong'onezo, na majivuno, na ghasia;

21. nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.

About 2 Wakorintho Chapter 12

Read 2 Wakorintho Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Wakorintho
Chapter: 12
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Wakorintho Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Wakorintho Chapter 12?

2 Wakorintho Chapter 12 is part of the Book of 2 Wakorintho in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Wakorintho Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2-wakorintho

  1. 2 Wakorintho Chapter 9
  2. 2 Wakorintho Chapter 8
  3. 2 Wakorintho Chapter 5
  4. 2 Wakorintho Chapter 11
  5. 2 Wakorintho Chapter 10
  6. 2 Wakorintho Chapter 7
  7. 2 Wakorintho Chapter 6

Explore More from Agano Jipya

  1. Wagalatia Chapter 4
  2. 1 Yohana Chapter 5
  3. Marko Chapter 7
  4. Matendo ya Mitume Chapter 1
  5. 2 Petro Chapter 2
  6. Wafilipi Chapter 1
  7. Waefeso Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. Ufunuo wa Yohana Chapter 3
  2. Wagalatia Chapter 3
  3. Waamuzi Chapter 8
  4. Yoshua Chapter 18
  5. Ezekieli Chapter 34
  6. 1 Yohana Chapter 2
  7. Hesabu Chapter 13
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *