2 Wakorintho Chapter 3

For English

Read 2 Wakorintho Chapter 3 Online

Read 2 Wakorintho Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wakorintho and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

2 Wakorintho 3

Sura 3

1. Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu?

2. Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;

3. mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

4. Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo.

5. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu.

6. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.

7. Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;

8. je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?

9. Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.

10. Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana.

11. Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.

12. Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;

13. nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;

14. ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;

15. ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

16. Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

17. Basi (Bwana) ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.

18. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

About 2 Wakorintho Chapter 3

Read 2 Wakorintho Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Wakorintho
Chapter: 3
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Wakorintho Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Wakorintho Chapter 3?

2 Wakorintho Chapter 3 is part of the Book of 2 Wakorintho in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Wakorintho Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2-wakorintho

  1. 2 Wakorintho Chapter 12
  2. 2 Wakorintho Chapter 8
  3. 2 Wakorintho Chapter 13
  4. 2 Wakorintho Chapter 10
  5. 2 Wakorintho Chapter 7
  6. 2 Wakorintho Chapter 6
  7. 2 Wakorintho Chapter 11

Explore More from Agano Jipya

  1. Yohana Chapter 12
  2. Wakolosai Chapter 1
  3. Wagalatia Chapter 6
  4. Warumi Chapter 4
  5. Waebrania Chapter 1
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 16
  7. Mathayo Chapter 28

Related Chapters & Readings

  1. Mhubiri Chapter 8
  2. Zaburi Chapter 118
  3. Mambo ya Walawi Chapter 9
  4. Hosea Chapter 14
  5. Isaya Chapter 48
  6. 1 Wakorintho Chapter 14
  7. Yeremia Chapter 40
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *