Read 2 Wakorintho Chapter 4 Online
Read 2 Wakorintho Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wakorintho and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Wakorintho 4
Sura 4
1. Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;
2. lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
3. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
4. ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
5. Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
6. Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
7. Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.
8. Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;
9. twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;
10. siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu.
11. Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.
12. Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu.
13. Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;
14. tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.
15. Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
16. Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
17. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
18. tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
About 2 Wakorintho Chapter 4
Read 2 Wakorintho Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wakorintho in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Wakorintho
Chapter: 4
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wakorintho. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Wakorintho Chapter 4 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Wakorintho Chapter 4?
2 Wakorintho Chapter 4 is part of the Book of 2 Wakorintho in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Wakorintho Chapter 4 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2-wakorintho
- 2 Wakorintho Chapter 8
- 2 Wakorintho Chapter 5
- 2 Wakorintho Chapter 11
- 2 Wakorintho Chapter 10
- 2 Wakorintho Chapter 9
- 2 Wakorintho Chapter 7
- 2 Wakorintho Chapter 6
Explore More from Agano Jipya
- 2 Wakorintho Chapter 7
- 1 Wakorintho Chapter 2
- Warumi Chapter 6
- Yakobo Chapter 5
- Ufunuo wa Yohana Chapter 2
- Yohana Chapter 1
- Wafilipi Chapter 3