Luka Chapter 17

For English

Read Luka Chapter 17 Online

Read Luka Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Luka in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Luka and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Luka 17

Sura 17

1. Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!

2. Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.

3. Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.

4. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

5. Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.

6. Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

7. Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?

8. Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?

9. Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

10. Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

11. Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.

12. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,

13. wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!

14. Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

15. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16. akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

17. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?

18. Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?

19. Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.

20. Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;

21. wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.

22. Akawaambia wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana wa Adamu, msiione.

23. Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate;

24. kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.

25. Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.

26. Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.

27. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

28. Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;

29. lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.

30. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.

31. Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.

32. Mkumbukeni mkewe Lutu.

33. Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.

34. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

35. Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

36. Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]

37. Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.

About Luka Chapter 17

Read Luka Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Luka in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Luka
Chapter: 17
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Luka. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Luka Chapter 17 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Luka Chapter 17?

Luka Chapter 17 is part of the Book of Luka in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Luka Chapter 17 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 4
  5. Waebrania Chapter 2
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 15
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 8

Explore More from Luka

  1. Luka Chapter 8
  2. Luka Chapter 22
  3. Luka Chapter 24
  4. Luka Chapter 12
  5. Luka Chapter 23
  6. Luka Chapter 21
  7. Luka Chapter 19

Related Chapters & Readings

  1. Hesabu Chapter 36
  2. Yeremia Chapter 6
  3. Mwanzo Chapter 9
  4. Hosea Chapter 6
  5. Waebrania Chapter 3
  6. Zaburi Chapter 29
  7. Ayubu Chapter 9
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *