1 Mambo ya Nyakati Chapter 22

For English

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 Online

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Mambo ya Nyakati 22

Sura 22

1. Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya Bwana Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa Israeli.

2. Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu.

3. Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani;

4. na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro wakamletea Daudi mierezi tele.

5. Daudi akasema, Sulemani mwanangu akali ni mchanga bado, na mwororo, nayo nyumba atakayojengewa Bwana haina budi kuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye fahari katika nchi zote; kwa hiyo mimi nitaiwekea akiba. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa.

6. Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba.

7. Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wangu.

8. Lakini neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;

9. tazama, utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake ;

10. huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakifanya imara milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.

11. Sasa mwanangu, Bwana na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya Bwana, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako.

12. Bwana na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya Bwana, Mungu wako.

13. Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.

14. Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.

15. Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanyiza kazi ya mawe na miti, na kila aliye mstadi kwa kazi yo yote;

16. ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye Bwana na awe pamoja nawe.

17. Tena Daudi akawaamuru wakuu wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema,

18. Je! Si Bwana, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwastarehesha pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za Bwana, na mbele ya watu wake.

19. Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta Bwana, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee Bwana Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la Bwana, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la Bwana.

About 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Mambo ya Nyakati
Chapter: 22
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22?

1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-mambo-ya-nyakati

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 1
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 25
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 2
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 15

Explore More from Agano la Kale

  1. Ayubu Chapter 22
  2. Amosi Chapter 4
  3. Zaburi Chapter 48
  4. Kutoka Chapter 32
  5. Zaburi Chapter 148
  6. Kutoka Chapter 4
  7. Isaya Chapter 28

Related Chapters & Readings

  1. 1 Samweli Chapter 21
  2. Zaburi Chapter 19
  3. Ayubu Chapter 39
  4. 2 Wafalme Chapter 20
  5. Yeremia Chapter 8
  6. Isaya Chapter 7
  7. 2 Samweli Chapter 17
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *