1 Mambo ya Nyakati Chapter 18

For English

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 Online

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Mambo ya Nyakati 18

Sura 18

1. Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti.

2. Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi wakaleta zawadi.

3. Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati.

4. Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.

5. Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu ishirini na mbili elfu.

6. Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.

7. Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri akazileta Yerusalemu.

8. Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.

9. Hata aliposikia Tou, mfalme wa Hamathi, ya kuwa Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, mfalme wa Soba,

10. akampeleka mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote.

11. Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki.

12. Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu.

13. Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda.

14. Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.

15. Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.

16. Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;

17. na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme.

About 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Mambo ya Nyakati
Chapter: 18
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18?

1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Mambo ya Nyakati Chapter 18 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-mambo-ya-nyakati

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 25
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 2
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 1
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 15
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 28

Explore More from Agano la Kale

  1. Ayubu Chapter 33
  2. Kutoka Chapter 3
  3. Ezekieli Chapter 36
  4. Esta Chapter 1
  5. Yeremia Chapter 22
  6. Habakuki Chapter 1
  7. Kutoka Chapter 35

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 11
  2. Zaburi Chapter 91
  3. Marko Chapter 14
  4. Yoshua Chapter 9
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 11
  6. Mwanzo Chapter 3
  7. Mambo ya Walawi Chapter 4
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *