1 Mambo ya Nyakati Chapter 23

For English

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 Online

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Mambo ya Nyakati 23

Sura 23

1. Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.

2. Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

3. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.

4. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;

5. na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

6. Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.

7. Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.

8. Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.

9. Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.

10. Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.

11. Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.

12. Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.

13. Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za Bwana, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.

14. Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.

15. Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.

16. Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.

17. Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

18. Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.

19. Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

20. Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.

21. Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.

22. Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

23. Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.

24. Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana, wenye miaka ishirini na zaidi.

25. Kwa kuwa Daudi alisema, Bwana, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;

26. wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.

27. Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.

28. Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya Bwana, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;

29. tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;

30. nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo;

31. na kumtolea Bwana sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za Bwana;

32. tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya Bwana.

About 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23

Read 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Mambo ya Nyakati
Chapter: 23
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23?

1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 is part of the Book of 1 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-mambo-ya-nyakati

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  2. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 6
  3. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 1
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 25
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 2
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 15
  7. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 28

Explore More from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 3
  2. Mwanzo Chapter 35
  3. Isaya Chapter 37
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 8
  5. Yoshua Chapter 19
  6. 2 Samweli Chapter 1
  7. Yeremia Chapter 16

Related Chapters & Readings

  1. Mathayo Chapter 3
  2. Mhubiri Chapter 2
  3. Ezekieli Chapter 40
  4. Matendo ya Mitume Chapter 15
  5. Ayubu Chapter 31
  6. Isaya Chapter 9
  7. Waamuzi Chapter 17
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *