Read Waefeso Chapter 3 Online
Read Waefeso Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Waefeso and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Waefeso 3
Sura 3
1. Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;
2. ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;
3. ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.
4. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
5. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6. ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
7. Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
8. Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
9. na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
10. ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
11. kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
12. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.
13. Basi naomba msikate tamaa kwa sababu ya dhiki zangu kwa ajili yenu, zilizo utukufu kwenu.
14. Kwa hiyo nampigia Baba magoti,
15. ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,
16. awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
17. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;
18. ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
19. na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
20. Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
21. naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.
About Waefeso Chapter 3
Read Waefeso Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Waefeso in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Waefeso
Chapter: 3
Testament: New Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Waefeso. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Waefeso Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Waefeso Chapter 3?
Waefeso Chapter 3 is part of the Book of Waefeso in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Waefeso Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano Jipya
- Waebrania Chapter 5
- Waebrania Chapter 1
- Waebrania Chapter 6
- Waebrania Chapter 4
- Ufunuo wa Yohana Chapter 1
- Waebrania Chapter 11
- Waebrania Chapter 10