1 Samweli Chapter 7

For English

Read 1 Samweli Chapter 7 Online

Read 1 Samweli Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Samweli and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Samweli 7

Sura 7

1. Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la Bwana, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la Bwana.

2. Ikawa, tangu siku hiyo ambayo sanduku lilikaa Kiriath-yearimu wakati ulikuwa mwingi; kwa maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Israeli wakamwombolezea Bwana.

3. Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.

4. Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia Bwana peke yake.

5. Samweli akasema, Wakusanyeni Israeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa Bwana.

6. Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia Bwana dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa.

7. Hata Wafilisti waliposikia ya kuwa wana wa Israeli wamekusanyika huko Mispa, mashehe wa Wafilisti walipanda juu ili kupigana na Israeli. Nao wana wa Israeli waliposikia, wakawaogopa Wafilisti.

8. Wana wa Israeli wakamwambia Samweli, Usiache kumlilia Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, kwamba atuokoe na mikono ya Wafilisti.

9. Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea Bwana sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia Bwana kwa ajili ya Israeli; Bwana akamwitikia.

10. Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; walakini Bwana akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.

11. Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hata walipofika chini ya Beth-kari.

12. Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa Bwana ametusaidia.

13. Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.

14. Nayo miji ile Wafilisti waliyokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa tena kwa Israeli, tokea Ekroni mpaka Gathi; na Waisraeli wakauokoa mpaka wake mikononi mwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Israeli na Waamori.

15. Naye huyo Samweli akawaamua Israeli siku zote za maisha yake.

16. Naye huenda mwaka kwa mwaka kuzunguka mpaka Betheli, na Gilgali, na Mispa; akawaamua Israeli mahali hapo pote.

17. Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu.

About 1 Samweli Chapter 7

Read 1 Samweli Chapter 7 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Samweli
Chapter: 7
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Samweli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Samweli Chapter 7 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Samweli Chapter 7?

1 Samweli Chapter 7 is part of the Book of 1 Samweli in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Samweli Chapter 7 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-samweli

  1. 1 Samweli Chapter 1
  2. 1 Samweli Chapter 11
  3. 1 Samweli Chapter 2
  4. 1 Samweli Chapter 6
  5. 1 Samweli Chapter 23
  6. 1 Samweli Chapter 22
  7. 1 Samweli Chapter 9

Explore More from Agano la Kale

  1. Ezekieli Chapter 7
  2. Yoshua Chapter 8
  3. Zekaria Chapter 5
  4. Ruthu Chapter 3
  5. Mithali Chapter 31
  6. Kutoka Chapter 28
  7. Mambo ya Walawi Chapter 5

Related Chapters & Readings

  1. Mambo ya Walawi Chapter 1
  2. Kutoka Chapter 5
  3. Ayubu Chapter 3
  4. Ezekieli Chapter 14
  5. Yohana Chapter 13
  6. 2 Wafalme Chapter 24
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *