Read Kumbukumbu la Torati Chapter 20 Online
Read Kumbukumbu la Torati Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Kumbukumbu la Torati 20
Sura 20
1. Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
2. Na iwe, msongeapo mapiganoni, kuhani na akaribie na kusema na watu,
3. awaambie, Sikizeni, enyi Israeli, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu mioyo yenu na isizime; msiche, wala msiteteme, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao;
4. kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
5. Na maakida na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine.
6. Ni mtu gani aliye hapa aliyepanda shamba la mizabibu, wala hajatumia matunda yake? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, yakatumiwa na mtu mwingine matunda yake.
7. Ni mtu gani aliye hapa aliyemposa mke wala hajaoa? Aende akarudi nyumbani kwake asije akafa mapiganoni, huyo mwanamke akaolewa na mume mwingine.
8. Tena maakida na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.
9. Itakuwa hapo watakapokwisha wale maakida kusema na watu, na waweke majemadari wa majeshi juu ya watu.
10. Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.
11. Itakuwa utakapokujibu kwa amani, na kukufungulia, ndipo watu wote watakaoonekana humo watakufanyia kazi ya shokoa, na kukutumikia.
12. Na kwamba hautaki kufanya amani nawe, lakini utafanya vita juu yako, ndipo uuhusuru;
13. na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga;
14. lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako.
15. Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya.
16. Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17. lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako;
18. wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu.
19. Wewe utakapohusuru mji siku nyingi kwa kufanya vita juu yake, upate kuutwaa, usiangamize miti yake kwa kupeleka shoka juu yake, kwani utaweza kula matunda yake; wala usiiteme, kwa maana huo mti wa kondeni, je! Ni mtu, hata ukauzuie?
20. Ila miti uijuayo si miti ya kuliwa iangamize, na kuitema; ukajenge maburuji juu ya mji ufanyao vita juu yako, hata uanguke.
About Kumbukumbu la Torati Chapter 20
Read Kumbukumbu la Torati Chapter 20 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 20
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 20 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Kumbukumbu la Torati Chapter 20?
Kumbukumbu la Torati Chapter 20 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 20 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from Kumbukumbu La Torati
- Kumbukumbu la Torati Chapter 34
- Kumbukumbu la Torati Chapter 6
- Kumbukumbu la Torati Chapter 25
- Kumbukumbu la Torati Chapter 21
- Kumbukumbu la Torati Chapter 3
- Kumbukumbu la Torati Chapter 1
- Kumbukumbu la Torati Chapter 16