Kumbukumbu la Torati Chapter 5

For English

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 5 Online

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kumbukumbu la Torati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kumbukumbu la Torati 5

Sura 5

1. Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia kuzitenda.

2. Bwana, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu.

3. Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai.

4. Bwana alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto;

5. (nami wakati ule nalisimama kati ya Bwana na ninyi, ili kuwaonyesha neno la Bwana; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema,

6. Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.

7. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

8. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.

9. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

10. nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

11. Usilitaje bure Jina la Bwana, Mungu wako; maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.

12. Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru.

13. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

14. lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.

15. Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.

16. Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

17. Usiue.

18. Wala usizini.

19. Wala usiibe.

20. Wala usimshuhudie jirani yako uongo.

21. Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.

22. Haya ndiyo maneno ambayo Bwana aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.

23. Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa kabila zenu, na wazee wenu,

24. mkasema, Tazama, Bwana, Mungu wetu, ametuonyesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi.

25. Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya Bwana, Mungu wetu, tutakufa.

26. Maana katika wote wenye mwili ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife?

27. Enenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema Bwana, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia Bwana, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda.

28. Naye Bwana akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; Bwana akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema.

29. Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele!

30. Enda uwaambie, Rudini hemani mwenu.

31. Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitanena nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.

32. Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na Bwana, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto.

33. Endeni njia yote aliyowaagiza Bwana, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

About Kumbukumbu la Torati Chapter 5

Read Kumbukumbu la Torati Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kumbukumbu la Torati
Chapter: 5
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kumbukumbu la Torati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kumbukumbu la Torati Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kumbukumbu la Torati Chapter 5?

Kumbukumbu la Torati Chapter 5 is part of the Book of Kumbukumbu la Torati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kumbukumbu la Torati Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Ayubu Chapter 4
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Kumbukumbu La Torati

  1. Kumbukumbu la Torati Chapter 26
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 33
  3. Kumbukumbu la Torati Chapter 27
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 28
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 24
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 30
  7. Kumbukumbu la Torati Chapter 31

Related Chapters & Readings

  1. Yohana Chapter 13
  2. Matendo ya Mitume Chapter 3
  3. Mathayo Chapter 7
  4. Zaburi Chapter 57
  5. Zaburi Chapter 147
  6. 2 Timotheo Chapter 1
  7. Mithali Chapter 30
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *