Read 1 Samweli Chapter 6 Online
Read 1 Samweli Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Samweli and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
1 Samweli 6
Sura 6
1. Basi, hilo sanduku la Bwana lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba.
2. Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Bwana? Tuonyesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake.
3. Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu.
4. Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa yatakuwa ya namna gani, hayo tutakayompelekea? Nao wakajibu, Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya mashehe wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya mashehe wenu.
5. Kwa hiyo mtafanyiza sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu waiharibuo nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.
6. Mbona, basi, mnaifanya migumu mioyo yenu, kama vile wale Wamisri, naye yule Farao, walivyoifanya migumu mioyo yao? Hata na hao, hapo alipokwisha kuwadhihaki, je! Hawakuwaruhusu watu, nao wakaenda zao?
7. Basi sasa jifanyizieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama zao na kuwatia zizini;
8. kisha, litwaeni hilo sanduku la Bwana, na kuliweka juu ya gari; na hivyo vitu vya dhahabu, mtakavyompelekea kuwa matoleo ya kosa, mvitie katika kasha kando yake; mkalipeleke sanduku, lipate kwenda.
9. Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni ajali iliyotupata.
10. Basi watu wale walifanya hivyo; wakatwaa ng'ombe wawili wakamwao, wakawafunga garini, na ndama zao wakawafunga zizini;
11. kisha wakaliweka sanduku la Bwana juu ya gari, pamoja na kasha lenye panya wa dhahabu na sanamu za majipu yao.
12. Na hao ng'ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kuume wala wa kushoto; na mashehe wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi.
13. Nao watu wa Beth-shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao bondeni; wakainua macho yao, wakaliona sanduku, wakafurahi sana kuliona.
14. Na lile gari likaingia katika konde la Yoshua wa Beth-shemeshi, na kusimama pale pale, palipokuwapo jiwe kubwa; basi wakaipasua miti ya lile gari, wakawatoa wale ng'ombe kuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
15. Nao Walawi walilishusha sanduku la Bwana, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa Bwana.
16. Na hao mashehe watano wa Wafilisti, hapo walipokwisha kuyaona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.
17. Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa Bwana; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja;
18. na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale mashehe watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la Bwana, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.
19. Basi Bwana aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la Bwana, wapata watu sabini, na watu hamsini elfu; nao watu wakalalamika, kwa kuwa Bwana amewapiga watu kwa uuaji mkuu.
20. Nao watu wa Beth-shemeshi wakasema, Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu? Naye atapanda kwenda kwa nani kutoka kwetu?
21. Nao wakatuma wajumbe waende kwa wenyeji wa Kiriath-yearimu, kusema, Wafilisti wamelirudisha sanduku la Bwana; basi shukeni, mkalichukue kwenu.
About 1 Samweli Chapter 6
Read 1 Samweli Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 1 Samweli
Chapter: 6
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Samweli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 1 Samweli Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 1 Samweli Chapter 6?
1 Samweli Chapter 6 is part of the Book of 1 Samweli in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 1 Samweli Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 1-samweli
- 1 Samweli Chapter 1
- 1 Samweli Chapter 4
- 1 Samweli Chapter 7
- 1 Samweli Chapter 27
- 1 Samweli Chapter 23
- 1 Samweli Chapter 16
- 1 Samweli Chapter 11
Explore More from Agano la Kale
- 2 Samweli Chapter 10
- Ezekieli Chapter 3
- Kutoka Chapter 38
- Mambo ya Walawi Chapter 22
- Hesabu Chapter 10
- Zekaria Chapter 3
- Zaburi Chapter 108