Read 1 Samweli Chapter 8 Online
Read 1 Samweli Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Samweli and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
1 Samweli 8
Sura 8
1. Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.
2. Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.
3. Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.
4. Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5. wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
6. Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.
7. Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
8. Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.
9. Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
10. Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.
11. Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
12. Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.
13. Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.
14. Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.
15. Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.
16. Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.
17. Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.
18. Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; Bwana asiwajibu siku ile.
19. Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;
20. ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.
21. Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana.
22. Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.
About 1 Samweli Chapter 8
Read 1 Samweli Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Samweli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 1 Samweli
Chapter: 8
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Samweli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 1 Samweli Chapter 8 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 1 Samweli Chapter 8?
1 Samweli Chapter 8 is part of the Book of 1 Samweli in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 1 Samweli Chapter 8 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 1-samweli
- 1 Samweli Chapter 1
- 1 Samweli Chapter 11
- 1 Samweli Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 6
- 1 Samweli Chapter 23
- 1 Samweli Chapter 22
- 1 Samweli Chapter 9
Explore More from Agano la Kale
- Hesabu Chapter 28
- Mithali Chapter 13
- Kumbukumbu la Torati Chapter 30
- 1 Wafalme Chapter 17
- Mambo ya Walawi Chapter 11
- Isaya Chapter 29
- Hesabu Chapter 32