1 Petro Chapter 2

For English

Read 1 Petro Chapter 2 Online

Read 1 Petro Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Petro and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

A+ A A-

1 Petro 2

Sura 2

1. Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.

2. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;

3. ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4. Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

5. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

6. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8. Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

9. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10. ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

11. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

12. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

13. Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;

14. ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.

15. Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;

16. kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.

17. Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

18. Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.

19. Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.

20. Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.

21. Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

22. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.

23. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.

24. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

25. Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

About 1 Petro Chapter 2

Read 1 Petro Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Petro in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Petro
Chapter: 2
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Petro. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Petro Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Petro Chapter 2?

1 Petro Chapter 2 is part of the Book of 1 Petro in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Petro Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-petro

  1. 1 Petro Chapter 1
  2. 1 Petro Chapter 5
  3. 1 Petro Chapter 4
  4. 1 Petro Chapter 3

Explore More from Agano Jipya

  1. Matendo ya Mitume Chapter 4
  2. Mathayo Chapter 5
  3. Marko Chapter 7
  4. 3 Yohana Chapter 1
  5. Mathayo Chapter 16
  6. Luka Chapter 1
  7. Yohana Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. Ezekieli Chapter 6
  2. 1 Wathesalonike Chapter 2
  3. Waamuzi Chapter 1
  4. Hesabu Chapter 27
  5. Zaburi Chapter 138
  6. Kutoka Chapter 30
  7. 1 Wakorintho Chapter 15
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *