Nahumu Chapter 2

For English

Read Nahumu Chapter 2 Online

Read Nahumu Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Nahumu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Nahumu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Nahumu 2

Sura 2

1. Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.

2. Kwa maana Bwana anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.

3. Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.

4. Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, Yanasongana-songana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.

5. Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.

6. Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa.

7. Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao.

8. Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.

9. Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo.

10. Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.

11. Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu?

12. Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwasongea wake zake nyama, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza mawindo.

13. Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.

About Nahumu Chapter 2

Read Nahumu Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Nahumu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Nahumu
Chapter: 2
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Nahumu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Nahumu Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Nahumu Chapter 2?

Nahumu Chapter 2 is part of the Book of Nahumu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Nahumu Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 6
  3. Isaya Chapter 2
  4. Isaya Chapter 14
  5. Isaya Chapter 3
  6. Isaya Chapter 8
  7. Isaya Chapter 7

Explore More from Nahumu

  1. Nahumu Chapter 3
  2. Nahumu Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 1
  2. Kumbukumbu la Torati Chapter 27
  3. 2 Petro Chapter 3
  4. Mwanzo Chapter 24
  5. Zaburi Chapter 82
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  7. Yeremia Chapter 48
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *