Zekaria Chapter 11

For English

Read Zekaria Chapter 11 Online

Read Zekaria Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zekaria and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zekaria 11

Sura 11

1. Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako.

2. Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

3. Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi! Kwa maana utukufu wao umeharibika; Sauti ya ngurumo ya wana-simba! Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.

4. Bwana, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,

5. ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe Bwana, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

6. Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema Bwana; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.

7. Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa.

8. Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.

9. Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe.

10. Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.

11. Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la Bwana.

12. Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu.

13. Kisha Bwana akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya Bwana.

14. Ndipo nikaikata vipande viwili fimbo yangu ya pili, iitwayo Vifungo, ili nipate kuuvunja udugu uliokuwa kati ya Yuda na Israeli.

15. Bwana akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu.

16. Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.

17. Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.

About Zekaria Chapter 11

Read Zekaria Chapter 11 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zekaria
Chapter: 11
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zekaria. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zekaria Chapter 11 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zekaria Chapter 11?

Zekaria Chapter 11 is part of the Book of Zekaria in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zekaria Chapter 11 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from zekaria

  1. Zekaria Chapter 6
  2. Zekaria Chapter 12
  3. Zekaria Chapter 7
  4. Zekaria Chapter 2
  5. Zekaria Chapter 14
  6. Zekaria Chapter 10
  7. Zekaria Chapter 4

Related Chapters & Readings

  1. Waamuzi Chapter 21
  2. Mambo ya Walawi Chapter 27
  3. Zekaria Chapter 13
  4. Yeremia Chapter 23
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 25
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 16
  7. Isaya Chapter 22
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *