Zekaria Chapter 4

For English

Read Zekaria Chapter 4 Online

Read Zekaria Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zekaria and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Zekaria 4

Sura 4

1. Na yule malaika aliyesema nami akanijia mara ya pili, akaniamsha, kama mtu aamshwavyo katika usingizi wake.

2. Akaniuliza, Unaona nini? Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake;

3. na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume walile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto.

4. Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?

5. Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.

6. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.

7. Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.

8. Tena neno la Bwana likanijia, kusema,

9. Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.

10. Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.

11. Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto?

12. Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao?

13. Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.

14. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.

About Zekaria Chapter 4

Read Zekaria Chapter 4 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zekaria
Chapter: 4
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zekaria. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zekaria Chapter 4 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zekaria Chapter 4?

Zekaria Chapter 4 is part of the Book of Zekaria in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zekaria Chapter 4 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from zekaria

  1. Zekaria Chapter 7
  2. Zekaria Chapter 10
  3. Zekaria Chapter 2
  4. Zekaria Chapter 11
  5. Zekaria Chapter 14
  6. Zekaria Chapter 5
  7. Zekaria Chapter 3

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 56
  2. Mathayo Chapter 13
  3. Ezekieli Chapter 44
  4. 1 Samweli Chapter 12
  5. Isaya Chapter 20
  6. 1 Samweli Chapter 22
  7. Isaya Chapter 31
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *