Zekaria Chapter 10

For English

Read Zekaria Chapter 10 Online

Read Zekaria Chapter 10 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Zekaria and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

A+ A A-

Zekaria 10

Sura 10

1. Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.

2. Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.

3. Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani.

4. Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila mtawala pamoja.

5. Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.

6. Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia.

7. Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana.

8. Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka.

9. Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi.

10. Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana.

11. Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.

12. Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina lake, asema Bwana.

About Zekaria Chapter 10

Read Zekaria Chapter 10 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Zekaria in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Zekaria
Chapter: 10
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Zekaria. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Zekaria Chapter 10 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Zekaria Chapter 10?

Zekaria Chapter 10 is part of the Book of Zekaria in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Zekaria Chapter 10 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from zekaria

  1. Zekaria Chapter 5
  2. Zekaria Chapter 3
  3. Zekaria Chapter 7
  4. Zekaria Chapter 6
  5. Zekaria Chapter 13
  6. Zekaria Chapter 11
  7. Zekaria Chapter 12

Related Chapters & Readings

  1. 2 Samweli Chapter 23
  2. Waebrania Chapter 11
  3. Mwanzo Chapter 43
  4. Yeremia Chapter 38
  5. Kutoka Chapter 23
  6. Yohana Chapter 6
  7. Hesabu Chapter 7
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *